HABARI KWA KIFUPI
TANGAZA HAPA
Qeene NTE Mchomvu
WAJUE WATANGAZAJI
WAPO RADIO
TANGAZA HAPA
Wajue watangazaji WAPO RADIO 98.0 MHZ
Copyright© WAPO RADIO
MERCY MOSES
NA
TAARIFA YA HABARI
W
A
P
O

R
A
D
I
O

T
U
M
E
L
E
N
G
A

K
U
K
U
H
A
B
A
R
I
S
H
A
HABARI KAMILI.

TANGA:
Jamii za wafugaji imetakiwa kujikita katika
uzalishaji wa Gesi  kwa kutumia kinyesi
kutoka katika mifugo,badala ya kutegemea
nishati ya kuni pamoja na mafuta ya taa.

Hayo yamesemwa Mjini Tanga na Waziri wa
Nishati na madini Mheshimiwa WILLIUM
NGELEJA wakati akifungua warsha ya siku
mbili ya wadau wa uzalishaji wa Gesi Nchini
yakiwamo makampuni binafsi.

Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea
kuwaunga mkono ikishirikiana na
wawekezaji wa teknolojia hiyo.

Mheshimiwa NGELEJA amesema sekta
binafsi inanafasi kubwa katika kufikisha
teknolojia hii ya gesi vijijini ambayo
itapunguza mahitaji ya umeme katika
maeneo mengi iwapo nguvu itaelekezwa
katika eneo hilo.

HABARI ZA KIMATAIFA.

RTIBLISI
Rais wa GEORGIA, MIKHEIL SAAKASHIVILI
amesaini Mkataba wa kukomesha mapigano
uliopendekezwa na Ufaransa kwa ajili ya
Umoja wa Ulaya na ambao unalenga
kumaliza mzozo wa kivita katika eneo
linalopigania kujitenga na GEORGIA, la
OSSETIA ya Kusini.

Mkutano huo umesainiwa wakati wa
mkutano kati ya Rais MIKHEIL
SAAKASHIVIL na Waziri wa mambo ya
kigeni wa Marekani BI CONDOLEEZA RISE
katika Mji Mkuu wa Georgia TIBLISI.

Akizungumza Juu ya Mkataba huo BI, RISE
amesema wakati umewadia sasa kwa Urusi
kujiunga na mkataba huo.

Aidha RISE ameongeza kusema kuwa
mkataba huo unapendekeza kutumwa katika
eneo ambalo wanajeshi wa kulinda amani
kwa kuanzia na waangalizi wa jumuiya  ya
usalama na ushirikiano barani ulaya OSCE.

JOHANNESBURG

Mkutano wa kilele wa siku mbili wa viongozi
wa Nchi wanachama wa jumuiya ya
maendeleo ya nchi za kusini mwa AFRIKA
SADC,umeanza leo Mjini JOHANNESBURG
Nchini Afrika ya Kusini ambapo jambo
kubwa linalozungumziwa ni mgogoro wa
Zimbabwe.

Rais ROBERT MUGABE,anashiriki katika
Mkutano huo kama rais wa Nchi.

Kiongozi wa Chama cha Upinzani Cha
Mageuzi ya Kidemokrasia cha MDC,
MORGAN TSVANGIRAI na kiongozi wa
Chama kilichojitenga na MDC ARTHUR
MUTAMBARA wanashiriki kama waangalizi
pekee.

Katika Mkutano huo ambao RAIS THABO
MBEKI wa Afrika ya Kusini atachukua
Uwenyekiti wa Jumuiya ya  SADC kutoka
kwa ZAMBIA, unarajiwa kubugikwa  hasa na
mazungumzo kati ya ROBERT MUGABE na
viongozi wa Upinzani juu ya uundwaji wa
Serikali ya Umoja wa Taifa.

Rais wa BOTSWANA,IAN KHAMA ambaye
hakuutambua Ushindi wa Rais ROBERT
MUGABE katika Uchaguzi wa Mwezi juni
mwaka huu ameususia Mkutano huo wa
mjini Johanesburg

BERLIN.

Kansela ANGELA MARKEL wa Ujerumani
ameikosoa Urusi kutokana na jinso
ilivyoshughulikia mzozo wa katika OSSETIA
ya kusini.


Markel ameitaka Urusi kuondoa majeshi
yake kutoka katika ardhi ya GEORGIA kama
hatua ya kwanza ya kufikia mkataba wa
kudumu wa kusimamisha mapigano.


Hata hivyo Rais wa Urusi MEDVEDEV
amesema kwamwe haitatokea majimbo ya
OSSETIA ya Kusini na AKHIBAZIA kuwa
sehemu ya Georgia.

MOSCOW.
Urusi imeonyesha kukasirishwa na mkataba
kati ya Marekani na Poland ambo utairuhusu
Marekani kuweka Ulinzi wa Makombora
yake Nchini POLAND.

Rais wa Urusi, DMITRY MEDVEDEV
ameyasema hayo katika Mkutano na
waandishi wa habari ambapo amesema
kuwa ulinzi huo wa makombora unaikusudia
Urusi.

Maafisa wa Marekani walikanusha mara
kadhaa wakisema mpango huo ni kwaajili ya
ulinzi wa Marekani na washirika wake dhidi
ya kile walichokitaja nchi za wasiojihehimu.

Maafisa wakuu wa POLAND na MAREKANI
walisaini Mkataba ambao utairuhusu
Marekani kuweka kwenye mwambao wa
bahari ya  BALTIC mitambo yake 10 ya
kunasa  na kuteketeza, makaombora kwa
upande wake,marekani iliahidi kuisaidia
Poland kuimarisha jeshi lake la anga.

PARAGUAY
Rais Mpya wa PARAGUAY, FERNANDO
LUGO amekula kiapo kuwa rais wa  Nchi
hiyo na hivyo kumaliza kipindi cha miongo
sita ya Utawala wa Chama cha
KONSEVATIVE cha KOLORADO PARTY.

Maelfu ya Raia wa PARAGUAY
amesherehekea wakati Askofu huyo wa
zamani akikabidhiwa madaraka katika Mji
Mkuu wa ASUNCION.

Akizungumza kwa kutumia Lugha zote mbili
za Kihispania na Guarani, ambayo ni lugha
yake ya asili Rais FERNANDO HUGO
ameahidi kupambana na rushwa na
umaskini.

Hata hivyo imeelezwa kuwa ahadi hizo ndizo
zilizomsaidia mwanasiasa huyo kupata
Ushindi katika Uchaguzi ambao Ulifanyika
mwezi Aprili mwaka huu.
.
MWISHO WA TAARIFA
YA HABARI KUTOKA
WAPO REDIO 98.0 FM.
TANGAZA HAPA
TANGAZA
HUUDUMA
YAKO
HAPA
TANGAZA HAPA