


| HABARI KWA KIFUPI |
| Qeene NTE Mchomvu |

| WAJUE WATANGAZAJI WAPO RADIO |

| WILSON KIBUGU NA KIPINDI CHA PATAPATA KINACHOANZA SAA 1.15 HADI SAA 1.45 |
| W A P O R A D I O T U M E L E N G A K U K U H A B A R I S H A |



| TANGAZA HAPA |

| TANGAZA HAPA HUDUMA YAKO |
| TANGAZA HAPA |
| Ni mwandishi wa habari, Mtangazaji, Mwandaaji na mtayarishaji wa vipindi Kazi za ziada zinazoshabihiana na kazi zangu ni pamoja na kuwa:- Mwalimu wa vijana, Ni mshauri wa vijana, Master of Ceremony – MC katika sherehe mbalimbali kama mikutano, harusi, send-off party, semina na tamasha. Pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili wilsonkibugu@wapotz.org |
| VIPINDI Kipindi cha ndoa na familia kinachorushwa hewani kila siku ya alhamisi saa 4.00-5.30 usiku ni moja ya vipindi ninachorusha hewani. Ni reporter wa kipindi cha Patapata kinachorushwa hewani kila siku saa 1.15 – 1.45 asubuhi Ni msomaji wa muhtasari wa habari unaosomwa kila siku saa 10.00-10.06 Ni msomaji wa taarifa ya habari inayosomwa kila siku saa 1.00-1.06 usiku Lengo la kipindi cha:- NDOA NA FAMILIA: Ni kipindi kinachoelimisha na kutoa ushauri mbalimbali kuhusu suala la zima la ndoa na familia Kutoa fursa kwa wanandoa kushiriki mazungumzo katika kipindi ili kutoa maoni pamoja na kushirikishana uzoefu katika yale ambayo wanandoa wanakabiliana nayo katika maisha ya ndoa kwamba ni namna gani wamefanikiwa kuwa na ndoa zenye amani na furaha. Kufanya mijadala na midahalo mbalimbali ili kuangalia changamoto mbalimbali zinaozowakabili wanandoa na jinsi ya kukabiliana nazo. Kukaribisha waalimu na wataalamu mbalimbali wanaoweza kuzungumza na kufundisha kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu ndoa na familia Jamii inavyofaidika na kipindi cha ndoa na familia: Wanandoa wanajifunza mambo mbalimbali yanayosaidia na kuwawezesha kuwa na ndoa zenye mafanikio, amani na furaha. Wanandoa ambao ndoa zao zinamgogoro wanaposikia hiki wengi wao wanajifunza mambo ambayo yanawasaidia kujitambua, kujua ni wapi wamekosea na warekebishe wapi ili kuwa na ndoa na familia zenye amani Hata wale ambao wamekuwa wamekata tama kutokana na maumivu, uchungu na vilio vinavyosababishwa na mgogoro ndani ya familia, wanaposikiliza kipindi hiki wanapokea uponyaji na faraja kutokana na elimu na mafundisho yanayofundishwa katika kipindi hiki. KIPINDI CHA PATAPATA Kipindi kinacholenga kuelimisha na kutoa taarifa ya habari mbalimbali kuhusu matukio mbalimbali yanayotokea katika jamii ikiwa ni pamoja na kuikumbusha jamii na viongozi wan chi kutambua wajibu wake katika utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo yao na Taifa kwa ujumla. FAIDA KWA JAMII Jamii inapata fursa ya kusikia na kufahamu taarifa na matukio mbalimbali yanayoendelea nchini, pia kinawawezesha jamii kujua wajibu wao katika mambo mbalimbali ambayo wanapaswa kutekeleza. TAARIFA YA HABARI Kinawezesha jamii kupata habari ambazo zinawasaidia kufahamu mambo mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii nchini na nje ya nchi. |
