GOSPEL CELEBRATION...
 | | Ukizungumzia waimbaji | | | waliofanikiwa haraka katika uimbaji wa muziki wa injili huwezi kumsahau Miriam Lukindo Mauki.
|
|
 | | Dada huyu wa kizigua, | | | mwenye sauti ya kipekee, aliyefanikiwa kupata mtoto mmoja kwenye ndoa yake, alifanikiwa kupata masomo ya awali Jijini Mbeya katika chuo cha Kilimo Uyole.
|
|
 | | Baada ya hapo, alihamia | | | mjini Moshi kujiunga na wazazi wake waliokuwa wakiishi mkoani Kilimanjaro.
|
|
 | | Aidha baada ya muda | | | alienda mjini Nairobi nchini Kenya katika kujiendeleza kimasomo.
|
|
 | | Binti huyu mtanashati, | | | kama anavyoonekana kwenye picha, awali hakujua kama yeye ana kipaji cha uimbaji, kutokana na sauti yake kuwa na mvuto; siku moja akiwa huko Nairobi, Mama mmoja alimwambia kuwa yeye anafaa kuwa muimbaji.
|
|
 | | Hivyo alimshauri kujiunga | | | na kikundi cha uimbaji chuoni hapo.
|
|
 | | Baada ya muda fulani | | | kuliandaliwa tamasha la uimbaji, Miriam pia alialikwa kwenda kuimba, na aliombwa aimbe wimbo wa Taifa la Tanzania.
|
|
 | | Aliimba vizuri sana na | | | watu walivutiwa na sauti yake kwa kuimba live, baada ya hapo aliamua kuingia hasa katika uimbaji, alianza kutunga nyimbo na wimbo wake wa kwanza uliitwa AMEN AMEN...
|
|
|