98.0 FM WAPORADIO
Simu
285 1 265
Kama uko
mikoani
022 285 1 265
SEMINA NA WARSHA MBALIMBALI
255 22 285 1 265
Mkutano mkuu utatanguliwa na warsha ya siku moja
itakayofunguliwa na naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi Dr. James Wanyancha siku ya Ijumaa Julai 25, 2008
asubuhi. Mada kuu ya warsha hiyo ni HAKI YA KIUCHUMI NA
KIJAMII; NAFASI YA MKULIMA MDOGO. (Economic and Social
Justice; the place of small holder farmers).

Washiriki wa warsha hii watapata nafasi ya kuchambua na
kujadiliana namna mkulima mdogo anavyoshirikishwa katika
haki za kiuchumi na kijamii hususan katika utekelezaji wa
miradi katika maeneo ya vijijini.

Warsha na mkutano mkuu wa 13 wa MVIWATA unatarajiwa
kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 250 wakiwemo wakulima
wanachama wa MVIWATA wapatao 200, kutoka mikoa yote ya
Tanzania bara na Zanzibar.

Wajumbe wengine waalikwa ni wawakilishi wa mashirika
wenza na MVIWATA toka ndani na nje ya Tanzania (yakiwemo
VECO, Oxfam, MSTz, FERT), wakurugenzi wa halmashauri za
wilaya na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali
wadau wa kilimo akiwemo rais wa shirikisho la wakulima
Afrika Mashariki (EAFF) na waandishi wa habari.

Aidha mkutano mkuu utaambatana na ajenda ya uchaguzi wa
wajumbe tisa wa bodi ya shirika la MVIWATA watakaokaa
madarakani kwa muda wa miaka mitatu ijayo.

Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) ni
chombo cha kuunganisha wakulima wadogo ili kuwa na sauti
moja katika utetezi wa maslahi yao ya kiuchumi, kijamii,
kiutamaduni na kisiasa.

Mtandao huu ulianzishwa mwaka 1993 na wakulima wadogo
wabunifu kwa lengo la kuweka utaratibu wa kubadilishana
mawazo,ujuzi na uzoefu miongoni mwa wakulima.

MVIWATA ilisajiliwa mwaka 1995 (hati ya usajili namba SO
8612) chini ya sheria ya vyama vya kiraia (Society
Ordinance). Ilisajiliwa kama Mfuko wa Dhamana mwaka 2000
na kusajiliwa kama asasi isiyo ya kiserikali mwaka 2007 (Hati
namba 1930) chini ya sheria ya ukubalifu ya mwaka 2002.
TANGAZA HAPA
KWA
KUTANGAZ
A HAPA
WASILIANA
NASI KWA
SIMU
No.
0754
567389
au
TUMA
E-MAIL:

waporadiofm@wapotz.o
rg
LAURA BONIVENTURE MSAMA
MOTO DAR, BALAA!
TANGAZA
HAPA
0754
567389
Shirika la Mtandao wa Vikundi
vya Wakulima Tanzania
(MVIWATA) litafanya mkutano
mkuu wa 13 siku za Ijumaa
Julai 25 na Jumamosi Julai 26,
2008 katika ukumbi wa Chuo
Kikuu cha Kiislam Morogoro.
Falsafa ya MVIWATA inajengwa katika misingi ya ushawishi
na utetezi wa maendeleo ya wakulima wadogo katika nyanja
za kiuchumi na kijamii; kuwezesha mawasiliano na kujifunza
kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwa wakulima.

Kimtandao, MVIWATA ni taasisi inayounganisha wakulima
wadogo, kuanzia ngazi ya mkulima mmoja mmoja, vikundi na
mitandao vijijini hadi mitandao ya kati (wilaya na mikoa) kisha
kitaifa.

Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa mpaka sasa ni pamoja;

1.        Mradi wa Maendeleo ya Masoko Vijijini Morogoro na
Dodoma (RMDP) uliofadhiliwa na serikali za Tanzania na
Ufaransa, uliotekelezwa 2002 hadi 2005 kwa ushirikiano na
FERT. Mradi huu uliwezeshwa kujengwa kwa masoko manne
katika vijiji vya Kibaigwa (wilaya ya Kongwa), Nyadira
(Mvomero), Tawa na Tandai (Morogoro)

2.        Mradi wa Kuendeleza Masoko Vijijini unaofadhiliwa na
Jumuia ya Ulaya na kutekelezwa kwa ushirikiano na shirika la
FERT katika mikoa ya Iringa, Tanga, Morogoro na Dodoma.
(umejenga masoko mawili katika vijiji vya Igagala (Njombe) na
Mkata (Handeni)

3.        Mradi wa Kuboresha Vyombo vya Kifedha vya
Wakulima uliotekelezwa kwa ushirikiano na taasisi za LVIA,
FERT na UMADEP katika mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro na
Morogoro. Ulifadhiliwa na Jumuia ya Ulaya. Mradi huu
umewezesha kuanzishwa na kuimarishwa kwa zaidi ya
SACCOS 30.

4.        Mradi wa Kuendeleza Utalii Vijijini unaotekelezwa kwa
ushirikiano na shirika la Agriterra la Uholanzi wilayani
Lushoto mkoani Tanga. Mradi huu unawaingizia kipato
wananchi kutokana na fedha zinazotolewa na watalii
wanaoishi kwa muda kwenye nyumba za wanakijiji ili
kujifunza tamaduni za kitanzania.

Gonga hapa kujua, nini kilichoamuliwa
kwenye warsha hii...
Kauli mbiu ya MVIWATA  
‘Mtetezi wa Mkulima ni Mkulima
Mwenyewe’.
TANGAZA
HAPA
Piga Simu
Namba
0754 567 389
Rais Jakaya
Mrisho
Kikwete
amesema

nini kwa
Wakulima
wakati wa
ufunguzi wa
soko la
wakulima
lililojengwa
kijiji cha
Igagala
wilayani
Njombe
mkoani Iringa
kwa gharama
ya zaidi ya
milioni 134
kwa
ushirikiano
wa Shirika la
Mtandao wa
Vikundi vya
Wakulima
Tanzania
(MVIWATA) na
shirika la
wakulima wa
nchini
Ufaransa
(FERT)...

==========
NDOA NA
FAMILIA:
Ni kipindi
kinachoelimisha na
kutoa ushauri
mbalimbali kuhusu
suala zima la ndoa
na
familia...
Shalom! Pre & Primary School: Mwaka jana wamefaulu kwa 100%
Shalom!
Pre &
Primary
School:
Mwaka
2007
wamefaulu
kwa 100%