KARIBU LACTAN BUGURUNI

October 13th, 2009

apostleencym
Apostle Ency Mwalukasa
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa WOWI/LACTAN
anawakaribisha katika huduma ya Ushauri,
Maombezi na Mafunzo. Huduma ipo karibu
na kituo cha basi Buguruni
Rozana kwa nyuma pembeni mwa shule ya
MOPAK ghorofa ya pili HEROS HOTEL kila Jumapili
saa 3.30 asubuhi
. Jumatano na Ijumaa saa 10.00 jioni
LACTAN – Light and Comfort to All Nations

HOUSEGIRL AELEZA MWAJIRI WAKE ALIVYOUAWA

March 9th, 2010

Charles Lyimo
Moshi Kilimanjaro
Tuesday, March 2, 2010 10:50 PM

waporadio.wapotz.org/yaliyotokea

SHAHIDI wa kwanza katika Kesi ya Mauaji inayomkabili raia kutoka nchini Ivori Cost Armand Guehi kwa kudaiwa kumuua mpenzi wake Angela Sama ameielezea mahakama kuu ya Tanzania kuwa wapenzi hao wamekuwa na ugomvi wa mara kwa mara na kudai kuwa mshitakiwa alikuwa akimlazimisha mpenzi wake kumpa pesa na anapopewa huendakutumia na wanawake wengine.

Shahidi huyo Dora Saimon Tarimo ambaye alikuwa yaya nyumbani kwa mshitakiwa amedai mahakamani hapo kuwa mnamo tar. 15/08/2005 marehemu aliondoka nyumbani na mumewe kuelekea kazini na mchana majira ya saa saba alirejea nyumbani na kumpa yaya huyo pesa nyingi za kigeni na kumwambia amuhifadhie na asimwambie mpenzi wake(Mshitakiwa).na kurudi
tena kazini

Shahidi huyo amedai kuwa usiku huo huo majira ya saa nne aliwasikia wapenzi hao wakigombana na ndipo alipomuona marehemu akitoka nje huku akiwa anavuja damu mdomoni alipomuuliza alimwambia kuwa amepigwa na mumewe hivyo anaelekea polisi.
.

Mbele ya Jaji
wa Mahakama kuu iliyopo Mjini hapa Jaji Moses G.Mzuna ,Shahidi huyo akiongozwa na wakili Mwandamizi wa Serikali kanda ya Kilimanjaro Vertas Mlay,alidai mahakamani hapo kuwa mara baada ya
kuona ni usiku sana alimshauri marehemu aende akapumzike kwa rafiki yake ndipo aende polisi siku inayofuata ushauri ambao Marehemu aliupokea na kwenda kwa rafiki yake na kukaa huko kwa kipindi cha wiki moja.

Shahidi huyo amedai mahakamani hapo kuwa kabla ya kutoweka nyumbani siku hiyo alishawahi kupigwa na kwenda kukaa kwa rafiki yake na baadae kurejea na kusuluhishwa na ndugu zake suluhu ambayo ilizaa matunda na waliendelea kuishi kwa pamoja lakini wakiwa bado wanagombana mara kwa mara.

Katika kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi Mkoani Arusha na Kilimanjaro kwa kuwa marehemu alikuwa alikuwa ni mtumishi wa umoja wa mataifa mkoani Arusha na Mwili wake kukutwa katika shamba la kahawa la mkufi shahidi aliendelea kudai kuwa mshitakiwa alikuwa hapendwi hata na wafanyakazi wenzake na marehemu

Shahidi huyo amezidi kudai kuwa mchana wa Augusti15 mshitakiwa alirudinyumbani na kwenda kupumzika na ilipofika jioni alimwagiza dukani kwenda kununua vocha ya simu na alipomletea hakujua alikuwa akiongea kitu gani kwani alikuwa akitumia lugha ya kifaransa.

Alizidi kudai kuwa hadi walipoamka kesho yake Marehemu(Angela)hakuonekana nyumbani na wala hakukuweza kumuuliza mpenziwe na badala yake alienda kazini kwake na kuambiwa hajaonekana kazini siku hiyo.

Hata hivyo shahidi
huyo amedai kuwa mara baada ya siku tatu Mpenziwe alikamatwa na siku nne baadae aliambiwa na Majirani kuwa Mwili wa Angela umeonekana katika shamba la Kahawa na Mkufi lililopo wilayani hai Mkoani hapa.

Mshitakiwa huyo mwenye kesi namba namba 40/2007 anatetewa na Mawakili wawili wakiongozwa na Eric Ng’imario akisaidiwa na Patricia Eric na ina jumla ya Mashahidi 14 ambapo tayari mashahidi wanne wameshatoa ushahidi wao na inaendelea kusikilizwa tena leo Machi 03.

…………Mwisho………….

Jump to Part 2…of the story

Whose mouths must be stopped

February 19th, 2010
Whose mouths must be stopped

Whose mouths must be stopped

Roulette (noun)
Gambling game with wheel

- A game in which a ball is rolled onto a spinning horizontal wheel divided into compartments, with players betting on which compartment the ball will come to rest in or a line of slits.

- Perforations made by a cutting tool on a sheet of paper or a tool with a toothed wheel used for making dots, e.g. in engraving, or for making perforations in paper, e.g. on a sheet of postage stamps

Necromancer: The practice of attempting influence, guessing the future or to communicate with the spirits of the dead in order to predict e.g.
• I could tell you what I think, but I’d only be guessing.
• She guessed the number before he turned the card over.
• form an opinion about something without enough evidence to make a definite judgment

Abominations means something that is immoral, disgusting, or shameful or a feeling of intense dislike or disapproval toward somebody or something

Divination:
Prediction, foresight, insight, foretelling, forecast
Witchcraft, the supposed use of magic to charm, delight, or captivate somebody or to cast a spell on somebody or something

Sorcerer means wizard, somebody who is believed or claims to have magical powers

WANA CCM WILAYANI MVOMERO WATAKA KATIBA IBADILISHWE

January 13th, 2010

Habari zaidi

Steven Mwikwabe

Vijana Choir wa BCIC Temeke na Steven Mwikwabe

WAKATI joto la kisiasa linaendelea kupanda nchini kuelekea uchaguzi mkuu,Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wilayani Mvomero wamekitaka chama hicho kufanya marekebisho ya kanuni na katiba kwa nafasi ya katibu wa wilaya kuwa ya kuchaguliwa badala ya kuajiriwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya Mbunge wa Jimbo hilo Sadiq Muradi katika mikutano ya kuhamasisha maendeleo,wanachama hao walisema makatibu hao ndio kichocheo kikubwa cha migogoro na vurugu majimboni hasa inapotokea kiongozi wa kitaifa kutaka nafasi ya uongozi katika jimbo husika.

Akionyesha jinsi katiba na kanuni za chama hicho zinavyokiukwa Selemani Msasa alisema viongozi wa ngazi za juu ndani ya chama hicho wanatumia nafasi zao kuteua makatibu watakao wabeba pindi watakapoonyesha nia ya uongozi hususani ubunge.

Vijiji vilivyodaiwa kutokewa na mkasa huo baada ya kuhutubiwa na Mbunge mnamo tarehe 16, 17 na 19 ni Kijiji cha Lusanga, Manyinga, Kigugu, Mlumbilo na Wami Dakawa ambapo Desemba 19, 20 na 21 kiongozi mmoja wa kitaifa (Amos Makala) akimgusa moja kwa moja Mbunge wa jimbo hilo alidaiwa kuhutubia Kigugu, Kilimanjaro, Kidudwe, Madizini, Kichangani, Mkindo, Lusanga na Manyinga.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wanakijiji wa vijiji vya Muhonda, Kichangani na Mkindo, mbunge wa jimbo hilo alisema jimbo la Mvomero limeingiliwa na mdudu mbaya wa siasa na kuwatahadharisha wananchi kuwa macho na wanaokuja na sera za kashfa.

Najua na mtashuhudia nimeitwa majina mengi ya kejeli eti kwa rangi yangu, ndugu zangu nina imani kuwa mnanifahamu mimi ni nani na nimefanya nini kwenu tangu 1997, hukumu mnayo ninyi, alisema Muradi.

Jimbo la Mvomero ni miongoni mwa majimbo ya uchaguzi mkoani Morogoro lililomegeka toka Morogoro Vijiji likiitwa Morogoro Kaskazini ambapo baada ya kumegeka kwake lilipata hadhi ya wilaya na kuitwa wilaya ya Mvomero hapo mwaka 2002.

Rose Mhando atwaa tuzo ya Wimbo Bora wa Injili

January 9th, 2010
Solomon Mukubwa na Waimbaji wa Praise and Worship ya BCIC

Solomon Mukubwa na Waimbaji wa Praise and Worship ya BCIC

Wimbo wa Mwimbaji maarufu Rose Mhando ujulikanao kama ‘Nibebe’ umeshinda tuzo ya wimbo bora wa Injili kwa mwaka 2009 baada ya kupigiwa kura zaidi ya 7000.00

Mwimbaji huyo alitangazwa kuwa mshindi na kujinyakulia zawadi ya kitita cha shilingi 200,000.00 mwishoni mwa mwaka 2009 katika fainali za shindano hilo lililoendeshwa kupitia television ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Wimbo huo ulichaguliwa kwa kura 7,234 ambazo zilipigwa na watazamaji katika shindano lililoendeshwa kwa njia ya kupiga kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia simu ya mkononi

Nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bw Solomon Mukubwa na wimbo wake ujulikanao kwa jina la ‘Mfalme wa Amanialiyepata kura zaidi ya 6,000 na kujinyakulia sh 100,000

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Bahati Bukuku kwa kuimba wimbo wa ‘Waraka wa Hamani’ uliopigiwa kura 6050 ambapo alitunukiwa zawadi y ash 50,000

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi kupitia TBC1, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta, aliwapongeza wasanii wa muziki wa Injili kwa kazi kubwa wanayofanya ya kufikisha ujumbe kwa jamii.

Hoteli iliyofunguliwa na Kikwete yabomolewa

December 24th, 2009

At BCIC Mbagala we are singing together

Siku mbili baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua hotel ya kitalii, Snowcrest iliyopo Ngulelo katika manispaa ya Arusha, ukuta wa hotel hiyo,umevunjwa.

Tukio la kuvunjwa kwa ukuta huo limetokea saa 11.30 alifajiri, desemba 21 mwaka huu chini ya usimamizi wa askari polisi wakiwa na silaha za moto,na imeezwa kuwa,sababu ya kuvunjwa kwa ukuta wa hotel hiyo ni kuwa ndani ya hifadhi ya barabara.

Akizungumza na waandishi wa habari,mkurugenzi wa Snowcrest ,Willfred Tarimo alisema kuwa amepata pigo kubwa juu ya tukio hilo na kwamba limemwathiri kwa kiasi kikubwa kibiashara kutokana na baadhi ya wateja wake zaidi ya 40 waliokuwa wamelala hapo, kuamua kutimuka kwa hofu.

Ameongea kuwa kufanyika kwa tukio hilo kuna chuki za kibiashara kwa lengo la kumwangusha kibiashara hasa kwa kipindi hiki cha mapumziko,ukizingatia hotel hiyo ni mpya na ima miezi mitatu tangu ianzake kutoa huduma.

Tarimo alikiri kupokea barua kutoka Tanroad ikimuelekeza kubomoa ukuta huo ambao inadaiwa ulikuwa ndani ya hifadhi ya barabara kwa urefu wa mita 10.

Alisema kuwa walishaarifiwa juu ya kuvunja kwa ukuta huo,hata hivyo ameeleza kushangazwa kwa unjwaji wa ukuta huo ambao umeenda sambamba na ufunguzi wa hotel hiyo uliofanya na Rais kikwete,hatua ambayo imeelezwa kumwingiza rais katika kashfa ya udhalilishaji.

Alihoji kuwa iweje uvunjwaji huo uanzie katika hotel yake ilihali,ujenzi wa barabara haujaanza rasmi huku maeneo mengi ya nyumba katika barabara hiyo yakiwa ndani ya hifadhi pasipo kubomolewa.

Alisema kuwa anaamini kubomolewa kwa ukuta huo kumetokana na chuki binafisi kutoka kwa mkurugenzi wa Tanroad mkoa wa Arusha,Deustedit kakoko ambaye alikiri kukwaruzana nae.

Aidha kwa upande wa meneja utawala wa Snowcrest ,Mark Diria alisema kuwa thamani ya uharibifu wa hotel hiyo ni mkubwa hata hivyo wanafanya tathimini ili kujua thamani kamili ya uharibifu.

Hata hivyo akiongea kwa njia ya simu meneja wa Tanroad, mkoani Arusha ,Deustedit Kakoko alisema kuwa hotel hiyo ilishaarifiwa kubomoa ukuta huo, lakini imekuwa ikikaidi na kushindwa kutoa ushirikiano.

Hoteli hiyo ya wazawa ilizinduliwa na Rais kikwete,Desemba 18 mwaka huu, huku uzinduzi huo ukienda sanjari na sherehe za kukata na shoka

Hoteli hiyo ina vyumba (83) na watumishi (120) imegharimu jumla ya dola za Kimarekani Milioni nane (milioni 8) ambapo sehemu kubwa ya fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo ya PTA.
…..Mwisho….

Semina ya Wake za Watumishi Yafana Dar

December 14th, 2009

Hatujaitiwa uadui na kulipizana kisasi;; Tumeitiwa upendo, furaha na amani
usiku na mchana, ukiruhusu mlango wa kuwa na uadui, ni wewe ndiye utakayepigwa katika kila
kona. Wewe ndio mchangiaji wa mumeo Mtumishi wa Mungu asifanikiwe katika kazi ya
Mungu. Na sasa piga magoti utubie ule uovu ulioufanya kiasi cha mumeo asifanikiwe
kiutumishi.

Hayo ni baadhi tu ya sehemu ya mahubiri ya Mchungaji Debora Kaisi, Mama Mchungaji Mtume Paul Kaisi wa Liko Tumaini kwa Mungu wa Uwanja wa Sifa Manzese wakati akifundisha katika semina ya wake za Maaskofu, Wachungaji, Wainjilisti na Mashemasi kutoka makanisa yote Dar es Salaam semina iliyofanyika katika kanisa la Living Water maarufu kama kanisa la Makuti
Kawe …

Mimi ni Anthony Joseph

November 9th, 2009

Copyright©WAPORADIO FMMimi ni Anthony Joseph, Mtangazaji na Mwandaaji wa kipindi chako ukipendacho cha yaliyotokea…

Habari nyingi za kipindi hiki zimekuwa zikivuta hisia za watu wengi sana na hii ni kutokana na jumbe tunazopokea na simu tunazopigiwa…

Mfano Bwana Alex wa Banana Dar es Salaam ameomba turuhusu watu mbalimbali wanaotokea kuwepo kwenye eneo la tukio wapewe ruhusa ya kutoa habari husika papo kwa papo ili kuleta ladha ya pekee katika kipindi hiki cha yaliyotokea…

Wewe unasemaje?

Pamoja na habari nyingi ulizowahi kuzisikia pengine unaweza kutuambia… ni habari ipi…iliyovuta sana hisia yako!?

Sisi tunaona habari ya Dodoma ya herufi M ilitushangaza sana! Je, wewe ni ipi?

Karibu WAPO RADIO FM 98.0 Mhz, karibu kipindi cha yaliyotokea kuanzia saa 1 jioni hadi saa 2 usiku

http://waporadio.wapotz.org/yaliyotokea.html

Hizi ni moja kati ya habari za Kilimanjaro
VIJANA nchini wametakiwa kufanya kazi za kujitolea zaidi
kwa kushirikiana na watu wa rika tofauti tfauti na kuachana na ubaguzi
wa rangi,dini,Ukabila,na hata utaifa ili kujiletea maendeeo katika
nchi yao…

ELIMU juu ya utunzaji wa mazingira katika jamii za
wananchi hususani waishio vijijini bado ni tatizo kutokana na wengi wa
wananchi kutokuelewa athari za uharibifu wa mazingira sanjari na
kutokufahamu vyema kuhusu faida za kuyatunza na kuyahifadhi mazingira…

Kwa kutoa maoni kuhusu taarifa hii nzuri
kutoka Mkoani Kilimanjaro Gonga hapa…

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo Aloyce Kimaro ametoa
msaada wa gari la kubebea wagonjwa katika hospitali
ya Kilema iliyopo chini ya Kanisa katoliki Jimbo la la
Moshi Mkoani Kilimanjaro gari lenye thamani ya zaidi
ya Sh. Mil.40….

Jiunge na Charles Lyimo kupata habari zaidi…

Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili

October 20th, 2009

Hatimaye Mkoa wa Shinyanga umejipatia wawakilishi wake watano ambao watashiriki kwenye shindano la kumsaka mwimbaji bora wa nyimbo za injili wa kanda ya ziwa.

Shindano hilo linalojulikana kwa jina la Zabuni Gospel Star Search limefanyika mkoani hapa oktoba 11 mwaka huu katika kanisa la FPCT Shinyanga kwa kushirikisha washiriki 15.

Shindano hilo lilianza kwa kutafuta kumi bora na baadaye kutafuta tano bora ambao watawakilisha Mkoa wa Shinyanga katika shindano la kumsaka Mwimbaji Bora wa nyimbo za injili wa kanda ya ziwa,ambalo linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Katika hatua ya tano bora msichana pekee aliyefanikiwa kuingia hatua hiyo ni Keflen Yona wa Shinyanga mjini,na wengine ni Philbert Joseph wa ,Kakozi Sadock, Dotto Nyilila wote wa Shinyanga mjini pamoja na Melicksedek Fikiri kutoka Wilaya ya Kahama.

Akiongea na wapo radio fm mwandaaji wa shindano hilo Florah Lawal ambaye pia ni miliki wa kampuni ya Florah Tarent Promotion and Rockland Promotion ya jijini mwanza amesema ameridhika na kiwango cha washiriki wote na angekuwa na uwezo angewachukuwa wote waliofanikiwa kuingia kumi bora.

Bi Florah ameongeza kwa kusema kuwa atahakikisha anawashawishi wadau watoe zawadi ya gari kwa mshindi wa kwanzana kuwa ametabiri zawadi hiyo itabaki Mkoani Shinyanga.

Kwa upande wake Tumsifu Rufutu ambaye alikuwa ni mmoja wa majaji wa shindano hilo amesema vijana wameonyesha uwezo mkubwa na anaimani kuwa shindano hilo litatoa mwimbaji bora wa nyimbo za injili.

Washiriki hao waliofanikiwa kuingia katika tano bira wanatarajia kuingia kambini mwezi desemba mwaka huu Jijini Mwanza tayari kwa mchujo wa kura kupitia kituo cha Television ambacho kitatangazwa baadae.

Mwisho……

Na Ester Sumira, Shinyanga.

October 20th, 2009

Dhambi ni kumuasi Mungu siyo kutofautiana na kiongozi wako

October 18th, 2009

Mr. Beda in a Prayer at BCIC Temeke

Mr. Beda in a Prayer

Mhariri, Gazeti la Msemakweli

Nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nitoe maoni yangu. Mungu akubariki wewe na watumishi wenzako wa gazeti hili.

Biblia inasema, “Watiini wenye kuwaongoza na kuwanyenyekea maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi,” Waebrania 13:17 Pia inasema wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao Waebrania 13:7

Kuwatii viongozi wa kanisa na wa kijamii ni agizo la Mungu. Kila amwaminiye Yesu anawajibika kuwatii. Biblia hata hivyo imetoa ufafanuzi na tahadhari. Pia ina mifano kadhaa kuhusu maana na mipaka ya huo utii. Kiongozi ni mtu mwenye dhamana ya kusimamia sheria, taratibu, wajibu na haki za jamii anayoiongoza

Ni mtu aliyepewa madaraka au mamlaka juu ya wanadamu wenzake. Aidha wamempa wao au amepewa moja kwa moja na Mungu na katika namna zote mbili Mungu anahusika. Mungu ndiye Mkuu juu ya viongozi na Mamlaka zote. Utii kwa maagizo ya una mipaka. Mfano, kiongozi wako wa kidini au kijamii atake kuwachukua watoto wako wadogo aende nao mahali usikokujua na kwa lengo usilolijua. Je, utakubali eti kwa vile yeye ni kiongozi wako?

Na akitaka kumchukua mumeo au mkeo; au gari, au shamba lako katika mazingira hayo tata; je, utamkubalia? Bila shaka utataka atoe kwanza hoja za msingi zitakazokutoa wasiwasi, na usiporidhika, naamini utakataa. Kiongozi au jopo la viongozi waliopo madarakani KIHALALI wanaweza kutoa maagizo HARAMU.

Inawezekana na imetokea mara nyingi. Na kwa sababu hiyo, ndiyo maana Mungu katika neno lake ametoa agizo, “kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao” Waebrania 13:7 Mwisho wa mwenendo ni nini? Je, ni pale unapozeeka na kukaribia kufa? HAPANA. Ni matokeo au athari za tabia, vitendo, misimamo, kauli, maagizo, mafundisho na imani yao. Walikotoka, walipo sasa na wanakoelekea kiimani

Nebukadreza, mfalme halali; maana imeandikwa, “Mungu wa mbinguni amekupa ufalme,” Danieli 2:37; alitoa amri haramu ya “kuiabudu… sanamu” Danieli 3:10 Shadrak, Meshak na Abednego wakakataa. Wakasema, “Sisi hatukubali kuitumikia miungu yako” Danieli 3:18 Mungu akawaunga mkono akawaokoa. Walipinga kwa njia za amani na kumheshimu mfalme, japo yeye aliona wamemdharau

Katika 1 Wafalme 21 Nabothi alikataa kuuza shamba la “urithi wa baba” zake kwa mfalme Ahabu. Alikataa matakwa haramu ya kiongozi halali. Nabothi aliuwawa. Shamba likachukuliwa. Lakini baada ya tukio hilo Mungu akamhukumu kifo Ahabu

Makuhani halali walitoa amri haramu kuwazuia mitume kumhubiri Kristo Yesu. “Petro na Yohana wakawaambia, kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia “Matendo 4:19-20

Wote, Petro na Yohana; Shadrak, Meshak na Abednego; pia Nabothi; hawakutenda dhambi kwa kule kukataa kutii maagizo haramu ya viongozi halali. Ndio maana Mungu aliukubali msimamo wao.

Elias S. Bilegeya
0765 653 985
Dar es Salaam

Click here to read Photos infos…